6 Februari 2022 - 18:47
UN: Imarati inasaidia magenge ya watu wenye silaha magharibi mwa Sudan

Umoja wa Mataifa umetoa ripoti yake maalumu na kusema kuwa, Umoja wa Falme za Kiarabu unayasadia magenge yenye silaha katika jimboi la Darfur la magharibi mwa Sudan.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Katika ripoti yake hiyo ya kila mwaka, Umoja wa Mataifa umesema pia kuwa, mamluki wanaodhaminiwa kifedha na Imarati nchini Libya ndicho chanzo kikuu cha kifedha za magenge mengi yenye silaha kwenye jimbo la Darfur nchini Sudan.

Katika ripoti yao hiyo, wataalamu wa Umoja wa Mataifa wamesema kuwa, awali misaada ya kifedha ya Umoja wa Falme za Kiarabu ilikuwa inatumwa kwa kundi linalojiita Jeshi la Taifa la Libya linaloongozwa na jenerali muasi Khalifa Haftar. Hivi sasa Imarati inalitumia kundi hilo kuyafikishia fedha magenge yenye silaha ya magharibi mwa Sudan.

342/